Posts

MALIMWENGU…..

Mapambo ya Njeri usiyapime naya Adhiambo wala ya Chelagat kwani ya Adhiambo ni ya kuvumiliwa na ya Chelagat ni ya bora niweke tu ilhali ya Njeri ni stare once but not look twice Ujinga ni kuwa unagraduate na umebeba mwaks kwa mfuko! Marehemu ni maiti iliyovishwa suti Avaaye minisketi haambiwi kaa skweya Apendaye nyimbo za reggae hakosi kuvuta bangi au ukipenda ‘weed’ Mwenye kitambi hakosi kuwa mfisadi tena wa hali ya juu. Maana ya neno mama ni kuwa ni mchumba wa baba. Atembeaye kwa champali hakosi kuwa ni mshamba wa bara tena mfidhuli. .Hapa Moi usiseme una mchumba, bibi au hata mke bali sema nina kirusha roho au stress releaser. Nawe janajike usiseme una chali bali sema una kichezea roho kwani si wewe pekee. ONYO; Demu wako akianza kukuita ‘baby’ chunga pengine kuna mtoto halisi amefunikwa na baada ya nusu mwaka na miezi tatu atawasili. Ujinga pamoja na utoto wa mtu hujitokeza anapougua maradhi ya frakaz. Babangu ni mzee lakini bado acheza kalongolongo na ha...

KUNI MBICHI!

                                                     Kuni mbichi ni msaliti wa moto. Torati zake ni kuufilisisha moto halafu kumshawishi chakula asihusiane na binadamu. Majipu yalikuwa yameshauteka mwili wangu nyara pasi huruma yoyote. Japo nilijizatiti niyakwaruze kwa, maji nayo yalikuwa yashamwagika na bila shaka kiu iliyonigubika ilizidi kuninyonga hata karibu nigeuke mwehu. Maisha nayo yalikuwa yametukodolea macho utadhani ibilisi alikuwa akiyaongoza. Chakula nacho kilikuwa nadra ja maji jangwani. Kuparara kwetu nako kulikuwa jambo jingine la kuzungumzia kwani macho yatakulipuka kwa mshangao ndugu. Miili yetu ilikuwa imebaki mifupa hata ladha ya kuwa binadamu ikawa shubiri. Kweli dunia si gunia la kuchezea ndugu na asiye...

KUOA SIOI TENA!

                                                                                    Janajike hili limeniparamia na kuniporomosha kihela pasi huruma yoyote. Nimekuwa shangingi wake kwa muda hata kumwacha nahisi kana kwamba nautema ulimwengu ulionilea. Ubabe wake umekuwa chanzo cha majonzi yangu huke matarajio yangu ya kimaisha nayo yamekuwa giza totoro. Demu huyu ni    ni jangili wa kimabavu kutokana na hila zake za kinyama. Vyombo vyangu vimekuwa vyake, nguo zangu nazo zimekuwa zake na si hayo tu, maisha yangu ameyamiliki hadi salamu nipatazo kutoka kwa akina dada wengine...