KUOA SIOI TENA!
Janajike
hili limeniparamia na kuniporomosha kihela pasi huruma yoyote. Nimekuwa
shangingi wake kwa muda hata kumwacha nahisi kana kwamba nautema ulimwengu
ulionilea. Ubabe wake umekuwa chanzo cha majonzi yangu huke matarajio yangu ya
kimaisha nayo yamekuwa giza totoro. Demu huyu ni ni jangili wa kimabavu kutokana na hila zake
za kinyama. Vyombo vyangu vimekuwa vyake, nguo zangu nazo zimekuwa zake na si
hayo tu, maisha yangu ameyamiliki hadi salamu nipatazo kutoka kwa akina dada
wengine huwa chanzo cha kukurupushwa naye. Nimekuwa mtumwa nyie ndugu zangu!
Kwanza
aingiapo chumbani mwangu salamu nizipatazo huacha akili yangu iki-hang. Marashi
ambayo huwa ameyamimina kwa makwapa yake kwa wakati mwingine hunifanya nizirai.
Kumbuka hata hayo marashi yalikuwa yangu hapo awali kwani niliyaiba kwa babangu
kutokana na ile hali ya kuwa hawezi nipa mapeni nikanunue. Baada ya salamu yake
kama kawaida huanza kunung’unika namna njaa invyombwaga, ‘haki baby njaa
inaniua, si twende Sowe.’ Moyoni kwa wakati huo najiambia ‘huyu mpumbavu hajui
sina pesa.’kudhihirisha ujinga wangu kwa maswala ya mapenzi nitampongeza kwa
hilo swala lake onevu. Baadaye hulia mvunguni mwa kitanda kwani ile shilingi
mia moja ambayo ingenipa gorogoro moja ya mahindi ya kusiaga ilikuwa
imeshanyakuliwa na hili jinamizi. Tuendapo
huko kununua chips huwa amenishika kwa mikono yake miwili kiunoni akiwaonyesha watu
hii ni mali yangu binafsi na hamjakaribisha.
Jamani
nimenyonywa damu na pia kimfuko. Mwili wangu umekuwa wa kijeneza karibu nafa.
Janajike hili limekuwa funza kwangu wa kuninyonya kimawazo pia. Anapopagawa
hujipachika viguo vifunikavyo sehemu core ilhali sehemu elective huziacha. Vitambaa
hivi hunitia kiwewe kwani huwa vina
maringo kwa sehemu nyingine za mwili kwani huzibagua tu. Nimekuwa mtumwa wa
kuuficha uchi wake kila mara. Dada huyo amen’roga mie mashangingi! Ni baradhuli
lisilo na bunduku bali bugdha za mama Mabruki wa Burundi. Pahala popote
lipitapo lawaroga hilo Janajike langu. Si mavazi, si umbo, si marashi, yote yajiuza
kivyao bila kujitembeza. Mapenzi yake yameoza na pia ni ya kidumba ambayo huwa
ni ya kunitia kiwewe. Amenisakama kwa namna zote hali ambayo imenilemaza na
kunifunga minyororo mazito kama ya nanga.
Jamani
kwa wale ambao wanataka kujitosa katika haya mazoeano ya mapenzi bandia nawashauri
mpitie kwangu huku Kibera yaani jumba la H lango la mwisho kabisa niwashauri ya
kuzingatia. Ikiwa watarajia tafadhalia lazima uwe tayari kwa yafuatayo; kutumia
hela zako kumshibisha hata ikiwa wahisi njaa, kumpigia simu kiholela hata
ikilazimisha kukopa okoa jahazi, kutokula
mboga nyakati hizo za mapenzi hafifu. Si
hayo tu, kuulizwa maswala balagha kila wakati, ‘uko wapi na uko na nani hapo,’ na
pia swala la kugombezwa wakati wowote ule hasaa ikiwa umekata mawasiliano naye.
Mapenzi ya hapa chuoni ni kama mchezo wa kalongolongo ambao huweza anza wakati
wowote halafu baadaye kwa muda mfupi tu walemazwa kwa vishindo. Kawaida
yanapoanza mabusu nashangwe za kikike huwa ndizo tarumbeta ya kitambulisho yake
ilhali yapogonga mwamba watu huchaniana nguo. Hapo ndipo watagundua ya kuwa walikuwa
wajinga. Utamsikia mmoja wao akisema, ‘kumbe sikujua kama yule Moshe ni mjinga
kiasi kile.’
Kwa
kweli mapenzi huweza kuwa kidonda na usipojihadhari utakuwa kidonda wewe mwenyewe.
Kwangu naona uhuni kwaniweza. Nanyi dada zangu kwaherini tutaonana ahera wakati
wa kichapo.
Comments
Post a Comment