KUNI MBICHI!
Kuni mbichi ni msaliti wa moto. Torati zake ni kuufilisisha moto halafu kumshawishi chakula asihusiane na binadamu. Majipu yalikuwa yameshauteka mwili wangu nyara pasi huruma yoyote. Japo nilijizatiti niyakwaruze kwa, maji nayo yalikuwa yashamwagika na bila shaka kiu iliyonigubika ilizidi kuninyonga hata karibu nigeuke mwehu. Maisha nayo yalikuwa yametukodolea macho utadhani ibilisi alikuwa akiyaongoza. Chakula nacho kilikuwa nadra ja maji jangwani. Kuparara kwetu nako kulikuwa jambo jingine la kuzungumzia kwani macho yatakulipuka kwa mshangao ndugu. Miili yetu ilikuwa imebaki mifupa hata ladha ya kuwa binadamu ikawa shubiri. Kweli dunia si gunia la kuchezea ndugu na asiye...